Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, Drake ameachia filamu yake mpya fupi yenye dakika 23 ya Please Forgive Me ambayo imetokana na albamu yake ya ‘Views’.

Filamu hiyo imetengenezwa kwenye mji wa Johannesburg, Afrika Kusini mwezi Julai. Watu kama Popcaan, Fanny Neguesha, Soni Chidiebere, na Kyla Reid wameshiriki kwenye filamu hiyo huku Anthony Mandler akiwa muongozaji.

Nyimbo kadhaa zilizopo kwenye albamu ya ‘Views’ zimeingizwa kwenye filamu hiyo ukiwemo wimbo wa ‘One Dance’, ‘Controlla’ na ‘Pop Style’.

Mwanzoni filamu hiyo iliotarajiwa kutoka Septemba 30, mwaka huu lakini imekuwa tofauti kutokana na sasa imeanza kupatikana kwenye mtandao wa Apple Music. Tazama kipande cha filamu hiyo hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *