Muigizaji nyota wa Bongo movie, Muhsen Hawadh ‘Dk Cheni’ amesema kuwa kwasasa ameacha kuigiza filamu kutokana na soko la filamu hizo kudorora hapa nchini.

Dr Cheni amesema ameamua kuacha kufanya filamu kwa muda mpaka pale soko la filamu litakapokuwa sawa kama ilivyokuwa hapo awali.

Muigizaji huyo mkongwe ameitaka serikali kuweka mazingira mazuri ambayo yatalinda kazi za wasanii kwa kuzuia maharamia wa kazi zao za sanaa.

Vile vile ameongeza kwa kusema kuwa wezi wa kazi za wasanii ni tatizo sugu kwa wasanii hapa nchini kwa hiyo serikali inatakiwa kuangalia kwa makini suala la kudhibiti maharamia wa kazi za wasanii.

Dk Cheni amedai wanaosambaza kazi zao ndiyo wezi wa kazi zao japokuwa taarifa zinaweza zikawa hazijaifikia serikali lakini watajitahidi kutoa ushirikiano kwa Mh.Nape Nnauye ili kuweza kuwakamata wezi kirahisi zaidi na kuokoa tasnia hii.

Muigizaji huyo alianza masuala ya uigizaji miaka ya nyuma wakati akiigiza katika tamthilia zilizokuwa zinarushwa na baadhi ya runinga nchini akiwa katika kundi la Kaole la jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *