Klabu za Borussia Dortmund na Legia Warsaw zimevunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kufungana jumla ya mabao 12.

Borussia Dortmund waliwafunga wapinzani wao kutoka Poland jumla ya goli 8-4 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Sidney Iduna Park nchini Ujerumani.

Walivunja rekodi iliyowekwa mabao 11 yalipofungwa mechi ambao Monaco waliwalaza Deportivo La Coruna 8-3 mwaka 2003.

Mabao saba yalifungwa dakika 22 za kipindi cha kwanza baada ya Dortmund kuongoza 5-2 kwa kipindi cha kwanza.

Legia ndiyo klabu ya kwanza kufunga mabao manne mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na bado kushindwa kwenye mechi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *