Rais wa Baraza la muungano wa Ulaya, Donald Tusk amesema kuwa maamuzi yanayofanywa na Donad Trump ni miongoni mwa chanagmoto zinazokumba muungano huo.

Amesema kuwa mabadiliko yaliofanyika nchini Marekani ni miongoni mwa vitisho kutoka nje vinavyojumuisha China, Urusi na Waislamu wenye itikadi kali kwa muungano huo.
Katika barua kwa viongozi 27 wa bara la Ulaya Tusk pia amesema kuwa anaamini kwamba wote wanakubaliana naye.

Taarifa kadhaa kutoka Washington zimesababisha maandamano dhidi ya Trump katika miji mikuu ya Ulaya.

Katika barua iliotolewa kabla ya kikao cha muungano huo huko Malta wiki hii, Tusk amesema kuwa utawala mpya wa Donald Trump umeiweka EU katika hali ngumu kwa kuwa unahoji sera ya kigeni ya Marekani ya miaka 70 iliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *