Rais mpya wa Marekani, Donald Trump ametoa mwaliko kwa waziri mkuu wa India Narendra Modi kutembelea nchini Marekani baada ya kufanya mazungumzo kwa njia ya simu.

Ikulu ya Marekani imemuelezea Mordi kama ‘rafiki wa kweli na mshirika kwenye kukabiliana na changamoto zilizopo duniani’.

‘Wamezungumzia fursa za kuimarisha ushirika baina ya Marekani na India kwenye maeneo mengi kama vile uchumi na ulinzi’.

Pia waziri huyo mkuu wa India amemkaribisha Trump nchini kwake.

Taarifa ya White House imesema kuwa rais Trump na Modi wamefikia makubaliano ya kusimama bega kwa bega kupambana na ugaidi duniani’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *