Mkali wa hip hop kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja maarafu kama ‘Janjaro’ amesema sababu inayomfanya azidi kuwa bora kwenye kazi zake ni ubunifu alionao kwasasa tofauti na hapo awali.

 Dogo Janja amesema kwa sasa yeye anakua kiumri hivyo hata uwezo wa kuandika mashairi yake unakua zaidi na kumafanya kila akitoa nyimbo inakuwa bora sana.

Janjaro ameongeza kusema kwamba sasa hivi anakua kwa hiyo hata uandishi wa mashairi yake unabadilika akitolea mfano wa nyimbo zake za nyuma kama Anajua, Siri zao, Ya moyoni, Mtoto wa Uswazi, My life mpaka nyimbo mpya ya sasa Kidebe utagundua kuna tofauti.

Pia Dogo Janja alizungumzia suala la kufanya show nyumbani kwao Arusha na kusema kwa sasa yeye ni msanii mkubwa hivyo show anayotaka kufanya lazima iandaliwe vya kutosha, lakini ni lazima akafanye show Arusha kwani ndio nyumbani kwao.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *