Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amesema kuwa siyo vizuri kwa msanii kuvaa nguo zinazofanana na shabiki wake.

Dogo Janja amesema kuwa huwezi kwenda jukwaani kuimba alafu wanakuja watu kama wanne kumshangilia alafu wawe wamevaa kama yeye inakuwa hakuna kilichobadilika

Ameongeza kuwa kinachompa kiburi kusema hivyo ni kwamba nguo zake huwa anaangiza kutoka nje ambazo huja kwa kupimwa uzito na si kama vijana wengine.

Pia amesema kuwa Hamna msaanii anayevaa au mwenye muonekano wa kistaa kama mimi East Africa, naamanisha ninachokisema, mimi kwanza hadi kuniona hivi nina watu ambao wamenizunguka.

Amesema kuwa Nina team kubwa ya watu imenizunguka kushughulika na muonekano wangu, hiyo ni nje ya management, mpaka miwani nina mtu ambaye anahusika nayo.

Mkali huyo kutoka Tip Top amesema kuwa “Mimi huwa sataki kuongea bei, nawatiaga watoto hasira ili wakatafute alafu wanakosa wanaishia kunitukana, hawapendi hasa mabishoo kwa sababu vitu ninavyoweka hawavikuti sehemu kwa hiyo wanapaniki.

Amemalizia kwa kusema kuwa hata cheni ninayovaa huwezi kuipata hivi hivi, nywele yangu tu ina gharama ya msosi wao wa siku, yaani ina gharama kama ndevu za Rick Ross.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *