Mwanamuziki wa hip hop, Dogo Janja amesema kuwa haogopi matusi kwenye mitandao ya kijamii kutoka mashabiki.

Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kwa kusema kwamba suala la matusi mitandaoni halimuongopeshi kutokana na mazingira aliyokulia lakini linapokuja suala la kuongezeana au kupunguziana vitu kupitia picha zilizopo mitandaoni huwa zinamuumiza na kumuogopesha.

“Suala la kutukanwa nimezoea sana, kwani sijaanza kutukanwa jana au leo kwa sababu mazingira niliyotokea mimi baba anaweza akamtukana mama mbele ya watoto. Ila linapokuja suala la mtu kukuwekea ‘shape’ kwenye mwili wako au kukupaka make up na kukugeuza kama mwanamke huwa naogopa sana pia zinaniumiza.

Pia rapa huyo kutoka Tip Top Connection amesema kwamba katika matumizi ya mitandao ya kijamii anaogopa sana watu wanapo hariri (edit) picha kuwa kuongeza au kupunguza kitu kwenye sura ya mtu.

Kwa sasa msanii huyo anatamba na wimbo wake unayokwenda kwa jina la ‘ukivaaje unapendeza’ iliyotengenezwa na prodyuza Daxo Chali Kutoka AM records.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *