Mwanamuziki wa Bongo fleva, Abdulaziz Abubakari maarufu kama Dogo Janja amesema kwasasa hayupo tayari kutoa albamu mpya siku za hivi karibuni mpaka hapo soko la kuuza muziki kwa mfumo wa albamu nchini utakapo kaa sawa.

Dogo Janja amesema kwamba hayupo tayari kutoa albamu mpya kwa sasa japokuwa lolote linaweza kutokea, bado menejimenti inaangalia upepo wa sokoni ulivyo, huwezi kutoa albamu kama hali ya sokoni ni mbaya.

Dogo Janja: Akiwa kwenye ndege na kiongozi wake wa Tip Top Connection, Madee
Dogo Janja: Akiwa kwenye ndege na kiongozi wake wa Tip Top Connection, Madee

Mbali na muziki Dogo Janja amesema anafanya biashara ndogondogo kwani huwezi kutegemea muziki pekee yake usawa huu maisha yalivyo magumu lazima azisake hata nje ya muziki.

Mwanamuziki huyo ambaye anatokea katika kundi la Tip Top Connection kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwa jina la ‘Kidebe’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *