Mwanamuziki wa hip hop kutokea pande za Tip Top Connection, Dogo Janja ametumia akaunti yake ya Instagram kuonesha gari jipya alilonunua aina ya ‘Raum’.

Dogo Janja ameonesha picha ya gari hiyo siku chache baada ya kuibiwa baadhi ya vitu kwenye gari lake aina ya Porte maeneo Sinza jijini Dar es Salaam.

Kupitia akaunti yake Instagram Dogo Janja ameweka picha akiwa juu ya gari huku akiandika maneno yaliyoonesha kumdisi mwanamuziki mwenzake, Young Killer.

Maneno hayo alioandika Dogo Janja yalisomeka kama ifuatatvyo “Don mess up with BUDABOSS!? ayah umeona dogo @youngkillermsodokii endelea kufuga icho kitoroli chako cha milion mbili…”

Wiki chache zilizopita Dogo Janja na Young Killer walikuwa kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV ambapo Young Killer alimtambia Dogo Janja kuwa amenunua gari kwa pesa yake mwenyewe.

Kutokana na kauli hiyo inaonesha kumuumiza sana Dogo Janja mpaka kupelekea kuandika maneno hayo ya kumkashifu Young Killer.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *