Mwanamuziki wa Bongo fleva, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa hadi sasa anajutia kuacha shule.

Dogo Janja amesema kuwa katika maisha yake anajutia kukosa shule na anasema katika kipindi ambacho alikuwa shule hakuwahi kupata uzoefu wa mitihani ya kujipama jambo ambalo lilichangia yeye kufeli shule na kushindwa kuendelea na masomo.

Mkali huyo amesema kuwa kilichsababisha yeye kuacha shule ni kufeli mitihani baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuhudhuria masomo mpaka kupelekea kufeli mitihani.

Dogo Janja alikuwa anasoma shule ya Sekondari ya Makongo iliyopo hapa jijini Dar es Salaam na kuishia kidato cha pili pekee.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *