Mkali wa ‘Kidebe’ Dogo Janja amejigamba kuwa hakuna msanii yoyote hapa nchini Tanznaia na ukanda wa Afrika ya Mashariki anayevaa na kupendeza kama yeye.

Dogo Janja maarufu kama Janjaro amesema kuwa kwasasa upande wa mavazi hana mpinzania kwani wengi wamekuwa wakivaa na kufanana na Wakongo ila yeye anavaa kinyamwezi.

Mwanamuziki huyo kutoka kundi la Tip Top Connection amesema kuwa yeye peke yake ndiye msanii anayevaa kinyamwezi kulingganisha na wengine.

Dogo Janja
Dogo Janja

Janjaro amesema kuwa watu wengine wanavaa rangi nyingi kiasi cha kuweza kumzimisha hata kinyonga hivyo hapaswi kulinganishwa na wasanii wengine.

Janjaro amesema kuwa ‘Hebu niangalie mimi sivai kama Mkongo navaa Kinyamwezi na katika wasanii peke yangu ndiyo ninavaa nikapendeza hata nikitokea mbele za watu sina haja ya kujitambulisha kuwa mimi ni msanii.

Hata hivyo watu katika mitandao ya kijamii wameanza kuponda maneno hayo ambaye hata yeye ameyaandika katika mtandao wake kwa kuhisi anatafuta kiki ya kuachia wimbo mpya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *