Mwanamuziki wa Bongo wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka kuhusu mahusiano yake, na kutoa sintofahamu kuhusu kutoka kimapenzi na muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya.

Dogo Janja ambaye mara nyingi hapendi kuzungumzia maisha yake binafsi, ameamua kusema kuwa msanii huyo anafaa.

“Irene ni mwanamke mzuri, anavutia, kila mwanaume anayejua mwanamke mzuri anafaa kuwa naye, ila kwa upande wangu mimi namkubali sana Irene Uwoya, kwani anaigiza vizuri, hivyo namkubali kwa kazi zake pia”.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za Irene Uwoya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Dogo Janja, ambapo watu wengi wamekuwa na mtazamo tofauti wakisema si sahihi kwani Irene Uwoya  ni mkubwa sana kwa Dogo Janja. Jambo ambalo Dogo Janja anaonekana kutoliafiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *