Wiki mbili zilizopita moja ya habari kubwa ilikuwa ikisumbua kwenye industry ya burudani ilikuwa ni video pamoja na maandishi ya majibizano yaliyoashiria ugomvi mkubwa baina ya mastaa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee a.k.a Vee Money na Shilole a.k.a Shishi Baby. Kwa mshangao wa wengi, majibizano hayo pamoja na kejeli kubwa walizokuwa wakionyeshana mastaa hao, wawili hao waliishia kufanya onyesho la pamoja kwenye ukumbi wa Bilicanas siku ya Jumapili iliyopita.

Je, nini kilitokea hadi upepo wa ugomvi ghafla ukageuka na kuwa urafiki hadi kufanywa kwa onyesho la pamoja? Je, ilikuwa ni njia ya kulitangaza onyesho hilo kwa kutumia promotion tool ijulikanayo zaidi kama STUNT au KIKI? Kile kilichokuwa ajabu kimewekwa wazi na staa, Vanessa Mdee aliyebainisha kuwa mastaa wengine wa Industry ya Bongo Fleva wanaofanya kazi katika ngazi tofauti ikiwemo wasanii, wacheza muziki ‘DJs’ na hata wazalishaji wa muziki ‘Producers’ walimtafuta kwa njia mbalimbali na kuhoji kilichokuwa kinatokea ‘majibizano yake na Shilole kupitia mitandao ya kijamii’. It is relieving to learn that, kuna wadau wa burudani ambao waliguswa sana na malumbano hayo. Shout out to wote walioguswa na kusaidia kupatikana kwa suluhu ya ugomvi kati ya mastaa Vanessa Mdee na Shishi Baby.

Many thanks to Dyna Nyange, Barnaba Classic….Chegge Chigunda, Fezza Kessy, Ruby na B12 kwa uchache.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *