Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amezindua gereza la wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Katika uzinduzi huo Mhandisi Masauni amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari wa jeshi hilo hapa nchini.

Amesema kuwa Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.

Akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa amesema kuwa ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa kushirikiana na wafungwa.

Kamishna Malewa amesema ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *