Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dkt. Willbroad Slaa amesema hana mpango wa kurudi Tanzania kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa hazina ukweli wowote.

Dkt. Slaa ametoa kauli hiyo baada ya kusambaa habari katika mitandao ya kijamii inayosema kuwa Slaa yupo mbioni kurudi nchini Tanzania.

Kwasasa Mwanasiasa huyo yupo nchini Canada alipoenda kwa masomo na makazi baada ya kuachia ngazi ya ukataibu ndani ya Chadema.

Habari zilizokuwa zinasambaa katika mitandao ya kijamii zilikuwa zinasema kuwa mwanasiasa huyo anaweza kurudi nchini na kujiunga na Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Lipumba ambao wote waliachia ngazi ndani ya vyama vyao.

Slaa alijiuzulu ukatibu mkuu wa CHADEMA na siasa za vyama baada ya CDM kumpokea Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kuwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa urais 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *