Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein amesema kuwa ni aibu kwa vijana wa Zanzibar kususia fomu za kugombea uongozi ndani ya CCM.

Dkt Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar ametoa kauli hiyo ya Dk Shein ametoa kauli hiyo baada ya Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mbamba aliyesoma taarifa ya mkoa huo mbele ya Dk Shein katika hafla maalumu ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Jimbo la Uzini akisema vijana wengi hawachukui fomu hizo.

Dk Shein amesema suala la msingi ni kuwa na uzalendo ambao ndiyo mwongozo sahihi katika kulinda heshima na nidhamu ya mtu kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.

Makamu huyo wa mwenyekiti wa CCM amesisitiza ajira ni changamoto kubwa kutokana na kuwa kwa sasa idadi ya watu visiwani humo ni kubwa hali inayosababishwa na Wazanzibari kuzaliana kwa wingi ikilinganishwa na nchi nyingine.

Awali, Sauda alimwambia Dk Shein kuwa pamoja na chama kutangaza uchukuaji wa fomu za uongozi, bado zimedoda matawini jambo linalohitaji nguvu ya pamoja ya viongozi wakuu kuwashawishi ili wazichukue.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *