Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema kuwa yeye ndiyo rais wa visiwa hivyo na Uchaguzi Mkuu mwingine utafanyika mwaka 2020.

Dk Shein amesema kuwa yeye ndio Rais wa Zanzibar na kueleza kuwa hakuna Baraza la Wawakilishi linalovunjwa ndani ya mwaka mmoja na kiutaratibu baraza hilo huvunjwa baada ya miaka mitano kwa sheria, taratibu na kanuni zake.

Aliyasema hayo kwenye Ukumbi wa CCM, Mkoa wa Mjini iliyopo Amani baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa vijana kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mpira wa Miguu kwa timu 18 za Unguja.

Dk Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar anayoiongoza yeye itaendelea kuwa madarakani na kueleza kuwa mazungumzo aliyoyafanya juzi kati yake na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni mazungumzo ya kawaida baada ya kumwita kwa lengo la kubadilishana mawazo na kueleza changamoto zilizopo katika majimbo yao.

Amesema akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi pia, ni sehemu ya baraza hilo na kwenda kuzungumza na wajumbe wa baraza hilo sio jambo jipya kwani ameshawahi kufanya hivyo kutokana na taratibu na kanuni zilizopo.

Pamoja na hayo, aliwasisitiza wanaCCM na wananchi kuwa hakuna baraza linalovunjwa asubuhi hivyo kauli hizo zinazozungumzwa na zinazosambaa ni za upotoshaji na zisizo na ukweli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *