Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya Iramba Mkoani Singida na kukagua huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya na Zahanati ya Kisimba wilayani humo.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla ameweza kubaini mapungufu mbalimbali ambayo ameagiza yapatiwe ufumbuzi ndani ya miezi mitatu.

Akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, ameweza kujionea huduma mbalimbali zitolewazo Hospitalini hapo hata hivyo ameagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanafunga mfumo wa ukusanyaji mapato wa malipo wa kisasa kwa njia ya kielektroniki.

Katika Zahanati ya Kisimba ambayo ipo umbali wa zaidi ya Kilometa 10, Dk. Kigwangalla ameweza kujionea huduma mbalimbali kwenye Zahanati hiyo ambayo ni mpya huku ikiwa msaada mkubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *