Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa elimu ya juu kulipa madeni ya mikopo kwa wakati.

Shein amesema kuwa wanufaika hao wanatakiwa kulipa mikopo kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar baada ya kumaliza masomo ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika na fedha hizo.

Dk Shein aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Afya, Mahmoud Thabiti Kombo wakati akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial University Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Pia ameitaka Bodi ya Mikopo kuvalia njua suala la marejesho ya mikopo kwa kutowaonea aibu wanufaika ili wengine waweze kunufaika na fedha hizo.

Vile vile amesema fursa ya mikopo bado ni ndogo hali inayochangiwa na uhaba wa fedha katika bodi, hivyo ni jambo la busara kwa wahitimu kuona umuhimu wa kurejesha fedha hizo kwa wakati.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *