Rais wa Zanzibar na mweneyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza Serikali ya Cuba kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika miradi ya maendeleo.

Dk amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Jorge Tormo katika Ikulu mjini Unguja viongozi hao walisisitiza haja ya kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo.

Kwa upande wake Balozi Tormo alimuhakikikishia Dk. Shein kuwa Cuba inathamini sana uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati yake na Zanzibar na kuahidi kuendelea kuudumisha.

Pia amesema kuwa miradi yote ya maendeleo inayoishirikisha nchi yake itaendelezwa kwa juhudi kubwa, huku akimweleza Dk. Shein kuwa nchi yake itafarajika kwa kuwapo ushirikiano katika sekta ya utalii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *