Aliyekuwa mgombea wa kwanza mwanamke kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Anna Senkoro anatarajiwa kuzikwa  kesho katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa familia ya marehem, Fred Sendim amesema kuwa taratibu za mazishi zitatanguliwa na ibada maalumu itakayoambatana na utoaji wa heshima za mwisho kuanzia saa saba mchana katika Kanisa la Winners lililopo Banana, Ukonga, jirani na kituo cha mafuta cha Oil Com.

dr_anna_claudia_senkoro

Sendim alisema Dk. Senkoro alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo na juzi saa 11 alfajiri alizidiwa na kupelekwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa matibabu na baadaye alihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alifikwa na mauti.

Dk. Senkoro aliyegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kupitia Chama cha APPT-Maendeleo, ameacha watoto watatu na wajukuu wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *