Aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Masaburi amelazwa hospitalini hapo akipatiwa matibabu, ambayo hata hivyo haijawekwa wazi anasumbuliwa na maradhi gani.

Mmoja wa madaktari wa kitengo cha dharura hospitalini hapo alithibitisha kupokewa kwa kiongozi huyo na kwamba amelazwa katika wodi ya Mwaisela.

Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alikiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo.

Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Neema Mwangomo alipoulizwa kuhusu kulazwa kwa Masaburi alisema hiyo ni siri ya mgonjwa na watu wake wa karibu.

Dk. Didas Masaburi alikuwa meya wa jiji la Dar es Salaam wakati wa Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, aligombea ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini aliangushwa na Saed Kubenea wa Chadema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *