Aliyekuwa DJ wa radio, David Mueller amekana madai yaliyotolewa na mwanamuziki Taylor Swift kwamba alimdhalilisha wakati alipokutana na mashabiki wake.

Ni mara ya kwanza kwa Bwana Mueller kuzungumzia kuhusu kile kilichotokea kabla ya tamasha la Detroit mwaka 2013.

Taylor amemshitaka kwa kumdhalilisha na kumtia aibu katika tukio hilo analosema lilimuacha lilimshitua na kumfanya ajitenge na watu.

DJ huyo wa zamani alifutwa kazi katika kituo cha kaunti cha muziki cha Colorado cobaada ya tukio hilo na sasa amezungumzia kuhusu mashtaka ya kisheria dhidi ya kipindi cha kituo cha redio cha Detroit, cha- Mojo In The Morning.

Tovuti ya Marekani TMZ umesambaza picha kutoka kwenye kipindi hicho kilichojulikana kama -meet and greet , ambazo David amesema hazikumuonyesha akimguza Taylor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *