Mwanamuziki maarufu nchini Marekani, Dj Khaled anatarajiwa kusherehesha tuzo za BET Hip-Hop Awards zitakazofanyika mwaka huu.

Dj Khaled alikuwa mshehereshaji katika tuzo za MTV Video Music Awards zilizofanyika wiki iliypita nchini Marekani na sasa amepata shavu lingine na BET,

Mkuu wa vipindi wa BET,  Stephen Hill ametoa tangazo hilo kupitia Snapchat na mwanamuziki huyo Dj Khaled amekubali mwaliko huo kwa moyo mmoja.

Pia Dj Khaled anawania tuzo nane zikiwemo DJ of the Year, MVP of the Year, na Hustler of the Year kwenye tuzo hizo za BET.

Show hiyo itarekodiwa Septemba 17  kwenye ukumbi wa Cobb Energy Performing Arts Centre katika mji wa Atlanta lakini inatarajiwa kurushwa kwenye Tv mbali mbali ifikapo Oktoba 4 mwaka huu.

Kupitia ukurassa wake wa Instagram Dj Khaled ameandika “They didnt want me to host the 2016 @bet Hip Hop Awards!! So guess what?? Im your host!! Tune in Oct 4th!! 8pm/7c #HipHopAwards #WeTheBest We have a lot of surprises!!!! Be ready!.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *