Mwanamuziki wa hip hop nchini Marekani, Dj Khaled ametangaza ujio wa album yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Grateful’ mwaka huu.

Album hiyo itakuwa ya 10 kutoka kwake ambapo amewashirikisha wanamuziki tofauti kwenye Album hiyo.

Jina la album hii limetokana na mapenzi ya watu kwake na kwa kazi zake ndiyo mana ameamua kuiita jina la Grateful akiwa na maana ya Kushukuru.

Wakati wa uzinduzi wa jina hilo palikuwa na wasanii kama Busta Rhymes, Kent Jones, P Diddy na Chance the Rapper.

Dj Khaled alitoa album yake ya ‘Major Key’, ambayo kwa sasa inawania tuzo ya Best Rap Album kwenye tuzo za Grammys zinazofanyika Jumapili Feb. 12.

Mpaka kwenye album hii ya 10 kutakuwa na wasanii kama vile Chance, Travis Scott, Mariah Carey, Bryson Tiller, Future na Alicia Keys.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *