Staa wa muziki nchini Marekani, DJ Khaled anatarajia kuachia albamu yake ya tisa inayokwenda kwa jina la “Major Key” ambayo itatoka Julai 29 mwaka huu.

Albamu hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo 14 ambazo zimerekodiwa chini ya studio ya Epic Records ambapo amewashirikisha wasanii tofauti maarufu nchini Marekani.

DJ Khaled: Akiimba jukwaani pamoja na rapa Lyl Wayne.

DJ Khaled: Akiimba jukwaani pamoja na rapa Lil Wayne.

Mastaa aliowashirikisha DJ Khaled kwenye albamu hiyo ni Jay Z, Future ,Drake, J. Cole, Nicki Minaj, Bryson Tiller, Chris Brown, Jeezy, Rick Ross, 2 Chainz, Busta Rhymes, Travis Scott, Lil Wayne, Wiz Khalifa, Wale, Nas na Meghan Trainor.

DJ Khaled ni mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla, amejizolea sifa kupitia nyimbo zake kutokana na kuwashirikisha wanamuziki wanaofanya vizuri nchini Marekani.

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *