Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lameck Ditto amefunguka kwa kusema kuwa katika maisha yake ya mahusiano ya mapenzi hajawahi kuumizwa na mwanamke.

Ditto amesema kwa sasa anaishi na mama watoto wake ambaye alianza nae mapenzi muda sana kwa hiyo hajawahi kuumizwa kabisa kutokana na kutopenda wanawake wengi.

Mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kutamba na kundi la Watu Pori amesema kuwa katika mahusiano hajawahi kuumizwa kabisa kwani hadi sasa hivi na mke na mtoto mmoja ambao wote anaishi nao.

Amesema kuwa ‘Mtoto wangu Lameck ana miaka 2 na kusema kweli tunafurahia maisha yetu na mungu akijalia tutafunga ndoa,”.

Muimbaji huyo ambaye pia ni mfanyabishara wa kilimo amekuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao hawategemei kiki kwenye muziki wao ila anatoa kazi nzuri kwa mashabiki zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *