Director Khalfani: Madirector Bongo hawana ubunifu

0
454

Muongozaji wa video za muziki nchini, Khalfani Khalmandro amesema kuwa kutokana na kazi zake anazozifanya kuwa bora haoni director anayesababisha kukosa usingizi kwa hofu kwenye kazi hiyo.

Director huyo amefunguka kuwa haoni ushindani katika soko la madirector wa sasa hapa Bongo na hivyo hakuna director wa kumnyima usingizi hata kidogo ndiyo mana kila kukicha kazi zake zinakuwa bora.

Muongozaji huyo amedai kuwa madirector wa Bongo hawana ubunifu, bali kila siku wanarudia vitu vile vile ambavyo vinafanyika kila siku.

Khalfani Khalmandro ni muongozaji wa video za wanamuziki wa Bongo fleva amefanya video nyingi ambazo zimefanya vizuri kwenye soko la Bongo fleva.

Video mpya alizofanya mkali huyo kwasasa ni Hela ya mkali Mdee kutokea pande za Tip Top Connection.

LEAVE A REPLY