Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Ommy Dimpoz amefungukia bifu yake na msanii mwenzake, Diamond Platinumz kuwa chanzo cha ugomvi wao ni Wema Sepetu.

Ommy Dimpoz ameyasema hayo leo wakati akifanyiwa mahojiano kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM

Dimpoz amesema mwanzoni walikuwa na urafiki mzuri na Diamond na walikuwa wakishirikiana mambo mengi kuhusu muziki wao lakini baadaye hali ilikuwa tofauti baada Diamond akaanza kumpoteza na kukwepa kufanya naye baadhi ya mambo kwa pamoja.

Dimpoz amesema hayo baada ya Diamond kusema mambo kadhaa kuhusu yeye wakati akifanya mahojiano jana kwenye kipindi hicho cha XXL.

Hayo yamekuja baada ya wawili hao kurushiana maneno machafu kupitia mitandao ya kijamii.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *