Klabu za ligi ya China zitaruhusiwa kuchezesha wachezaji watatu wa kigeni kwa kila mechi kwenye msimu mpya utakaoanza mwezi machi mwaka huu.
Sheria hiyo imekuja ili kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa kwenye ligi hiyo kutoka barani Ulaya ili kukuza wachezaji wa ndani ya nchi hiyo.
Hapo awali sheria ilikuwa “4+1” mana yake wachezaji wanne wa kigeni kutoka taifa lolote na mchezaji mmoja kutoka ndani ya bara la Asia kwenye kikosi.
Klabu hiyo ya Tianjin Quanjian inafundishwa na naodha wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Fabio Canavaro.