Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amemuacha mshambuliaji wake Diego Costa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Leicester City kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza katika uwanja wa King Power leo.
Maamuzi ya kocha huyo huyo kumuacha Diego Costa ambaye ndiyo kinara wa magoli katika ligi hiyo kutokana na mshambuliaji huyo kutofanya mazoezi na wachezaji wenzake kwasababu anataka kuihama timu hiyo baada ya kuletwa ofa kutoka China.
Costa alipata ofa hiyo kutoka China inatakayomfanya kupokea kitita cha pauni milioni 30 kwa mwaka,mshahara ambao ungemfanya kua mmoja kati ya wachezaji ghali duniani.
Baada ya kufika mezani kwa Ofa hiyo Diego Costa akashindwa kuwa katika hali yake ya kawaida na kushindwa kufanya mazoezi na wenzie kama ilivyo kawaida.