Mwanamuziki wa Hip Hop nchini Marekani, Sean John Combs maarufu kama ‘P. Diddy’ ameendelea kuongoza orodha ya marapa wa nchi hiyo wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Forbes inasema kuwa Diddy kwa kipindi cha mwaka mmoja ameingiza kiasi cha dola milioni 62 hadi sasa.

Kiasi cha fedha kinachoingizwa na mwanamuziki huyo kinatokana na matangazo aliyongia na baadhi ya makampuni nchini Marekani ambayo yanamuingizia mkwanja mrefu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Pia mwanamuziki huyo anamiliki lebo yake mwenyewe inayojulikana kama ‘Bad Boy’ ambapo anamiliki baaddi ya wasanii ndani ya lebo hiyo ambapo pia inamuingizia mkwanja wa kutosha kabisa.

Nafasi ya pili imeshikiliwa na rapa Jay-Z ambapo kwa mwaka mmoja amefanikiwa kujikusanyia mkwanja wa dola milioni 53. 5 hadi sasa.

Jay-Z pia anamiliki lebo ya muziki ambayo pia inamuingizia mkwanja wa kutosha ambapo amefanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye ordha hiyo.

Tazama orodha kamili ya marapa wanaoingiza mkwanja mrefu zaidi kwa kipindi cha mwaka mmoja nchini Marekani.

Je kuna rapa aunayemkubali ambaye yupo kwenye oradha hii?

1. Diddy – $62 million
2. Jay Z – $53.5 million
3. Dr. Dre – $41 million
4. Drake – $38.5 million
5. Wiz Khalifa – $24 million
6. Nicki Minaj – $20.5 million
7. Pitbull – $20 million
8. Pharrell Williams – $19.5 million
9. Kendrick Lamar – $18.5 million
10. Birdman – $18 million
11. Kanye West – $17.5 million
12. DJ Khaled – $15 million
13. A$AP Rocky – $14.5 million
14. J. Cole (Tie) – $14 million
15. Lil’ Wayne (Tie) – $14 million
16. Macklemore & Ryan Lewis (Tie) – $14 million
17. Snoop Dogg $12.5 million
18. Eminem – $11 million
19. Swizz Beatz – $10.5 million
20. Ludacris (Tie) – $10 million
21. Rick Ross (Tie) – $10 million

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *