Mwanamke wa Kinyarwanda, Diane Rwigara ametangaza nia ya kuwania Urais nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .

Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.

Mtangaza nia huyo amesema kuwa kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha.

Pia amesema kuwa kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.

Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *