Miss Kinondoni 2016, Diana Edward Lukumai aimefanikiwa kuibuka kidedea kwa kutwaa taji la Miss Tanzania 2016.

Diana ameibuka kidedea na kuwabwaga wenzake 30 waliokuwa wanashiriki shindano hilo la urembo nchini.

Ushindi huo unamfanya Diana kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo wa dunia.

Shindano hilo kwa mara ya kwanza limefanyika jijini Mwanza katika ukumbi wa Rock City Mall.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *