Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Diamond Platnumz amesema kuwa msanii Saida Kalori alimwambia kwamba anatamani kufanya naye kazi kabla ajawaza kufanya nyimbo ya Salome.

Diamond amesema kwamba wimbo ‘Salome’ ambao unaendana kabisa na wa Saida Kalori ulipata Baraka zote kutoka kwake na walipowasiliana kwa njia ya simu alimwambia anatamani kufanya naye kazi.

Pia Diamond amesema amefurahishwa na namna mashabiki kutoka ndani na nje ya nchi walivyoupokea vizuri na kusisitiza kwamba wimbo huo kutokana na mahadhi yake unafaa kupigwa katika nchi yoyote ndiyo maana mavazi yake yalizingatia tamaduni za makabila mbalimbali ndani na nje ya nchi ndani ya bara la Afrika.

Diamond ameufanyia remix wimbo wa Said Kalori uitwao Maria Salome lakini Diamond wake unaitwa Salome ambao amebadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo huo wa Saida Kalori.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *