Shusha pumzi, hayakuwa mashindano na wala hakukuwa na lengo la kuwafanya Diamond Platnumz a.k.a Dangote na Ali Kiba a.k.a King ‘watoane jasho’!

Mastaa hao wa Tanzania walijikuta wakifanya shoo kwenye jukwaa moja huko Mombasa nchini Kenya wiki iliyopita ingawa ‘kila mmoja alifanya kwa wakati wake’.

Shoo hiyo ‘iliyojaza nyomi la kutosha’ ilitarajiwa na mashabiki wengi kutumika kama kielelezo cha kupima ubora wa wasanii hao wanapokuwa jukwaa moja lakini katika hali ya kushangaza waandaaji wake wakamfanya Ali Kiba kuwa ‘surprise performer’.

Ingawa kwa sehemu kubwa ya watanzania walidhani kuwa shoo hiyo ilikuwa ya Diamond Platnumz alikini wenzao wa Kenya waliambiwa mapema kuwa King Kiba atakuwa jukwaa moja na Dangote.

Ali Kiba anadaiwa kufanya makeke yake baada ya kumalizika kwa shoo ya Diamond Platnumz hali iliyozua tetesi kuwa staa huyo wa WCB amemkimbia King Kiba jukwaani lakini kwa mujibu wa meneja wa Diamond Platnumz, Sallah, team nzima ya WCB haikuwa na taarifa na ujio wa Kiba na wala haikujulishwa iwapo sta huyo wa ngoma ya ‘AJE’ atatumia jukwaa hilo hilo alilolitumia Diamond Platnumz kuwapa burudani fans wa Kenya.

Sallam amenukuliwa akisema:
‘Hatukufahamu chochote kuhusu ujio wa Kiba kwasababu tangu awali hatukuambiwa kwamba AliKiba atakuwa kwenye show’.

‘AliKiba alikuja kama msanii wa surprise kwa mashabiki wa Mombasa na hiyo inaonyesha namna muziki wa Tanzania unavyokubalika nje ya mipaka yake’.

‘Waandaaji ndio wenye maamuzi ya kuwaita wasanii hivyo sisi tulienda kutekeleza kile ambacho mkataba wetu ulitutaka kufanya bila kuzingatia nani mwengine amealikwa’.

Je, kunahitajika kuandaliwe onyesho la pamoja la King Kiba na Diamond Platnumz?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *