Mwanamuziki nyota wa Bongo fleva, Diamond Platnumz anatarajia kuingiza sokoni bidhaa ya manukato itakayojulikana kama ‘Chibu Perfume’ hivi karibuni.

Mkali huyo ameonesha manukato hayo kupitia video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu bidhaa yake hiyo.

Mwanamuziki huyo amefuata nyayo za wakali kama Jennifer Lopez na Nicki Minaj ambao tayari wameingiza sokoni manukato yao na kufanikiwa kuingiza pesa nyingi kutokana na manukato hayo.

Manukato hayo yanaweza kumsababishia mwanamuziki huyo kuingiza kiasi kikubwa cha pesa kutokana na umaarufu wake wa ndani na nje ya nchi.

Diamond Platnumz uhenda akafuata ushauri wa mwanamuziki mwenzake GK aliyemshari kufanya biashara kwasababu muziki unapanda na kushuka huwezi kuwa juu miaka yote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *