Diamond Platnumz apewa heshima Marekani

0
77

Mwanamuziki Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekabidhiwa jezi na timu ya Washington Football Team ya American Football nchini Marekani.

Diamond amekabidhiwa jezi hiyo iliyoandikwa Platnumz yenye namba 99 mgongoni ikiwa ni ishara ya kuthaminiwa na timu hiyo kubwa Duniani.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram Washington wamethibitisha hilo kwa kupost picha za Diamond akiwa na jezi yao ikiambatana na ujumbe uliosomeka Diamond repping the Burgundy & Gold.” Washington NFL.

Timu ya Washngton inashikilia nafasi ya pili (2) kwenye msimamo wa Ligi ya mpira wa Marekani msimu huu.

Diamond kwa sasa yupo nchini Marekani kwa ajili ya tour yake ya muziki ambapo anatarajia kwenda kupiga shoo Minnepolis kesho Ijumaa, October 15 na Denver, October 16, Jumamosi.

LEAVE A REPLY