Wimbo ‘Kidogo’ wa Diamond Platnumz aliyowashirikisha PSqaure umeshinda tuzo ya African Entertainment Legend Awards (AELA), zilizotolewa nchini Nigeria usiku wa kuamkia leo.

Wimbo huo umeshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Best Collaboration (Africa) kwenye tuzo hizo zinazoandaliwa nchini Nigeria.

Wimbo huo umejizolea umaarufu nchini Tanzania pamoja na nje ya nchi kutokana na ubora wa mashairi katika wimbo huo ambao umepata nafasi ya kuangaliwa mara nyingi sana kupitia mtandao wa Youtube.

Diamond Platnumz si mara ya kwanza mwaka kupata tuzo kwani ameshinda tuzo za AFRIMA zilizotolewa mapema mwezi huu pia alikuwemp kwenye tuzo na MTV MAMA lakini ameshindwa kufanya vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *