Producer aliyefanikiwa kutoa vichwa vikali tupu kwenye Bongo Fleva kuanzia miaka ya 90, P Funk Majani anaamini Diamond Platnumz anajichimbia shimo la kupotea.

Kwanini?

Staa huyo anaamini kuwa Diamond Platnumz hawekezi kwenye kujenga mazingira ya mashabiki wake kumis na kumhitaji na badala yake amekuwa akiwashughulisha mno fans wake kwa kila siku kuwepo kwenye macho na masikio yao.

Kama hajaachia ngoma mpya basi atakuw akwenye social media ana trend akikosekana huko basi WCB itakuwa ina jambo fulani ambalo yeye atakuwa mbele kabisa.

Kwa mtazamo wa majani fans watamchoka SIMBA ndani ya muda mfupi kwakuwa hawataona jipya kutoka kwake.

Pamoja na personality yake pia Majani amewashauri WCB hususani Diamond mwenyewe kuwa label yake ni lazima itengeneze mazingira ya kubadilisha ladha ya muziki kutoka kwenye label hiyo badala ya wasanii wote na ladha za ngoma zote ‘kufanana kila kitu’.

Kazi kwako Simba, mkongwe katoa ushauri ni jukumu lako kuzingatia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *