Ni jibu kwa Ali Kiba baada ya kuomba Sony waachie ngoma zake?

Maana ngoma za Platmnumz zinazidi kupaa ughaibuni.

wazi kuwa mchuano wa majogoo wawili wa jiji la Dar es Salaam, Ali Kiba a.k.a KING na Diamond Platnumz a.k.a SIMBA kwa mwaka 2017 utakuwa mkali sana.

Baada ya kampuni ya Sony kumzawadia KING Kiba kwa ngoma yake ya AJE kufikisha views zaidi ya milioni 5 kwenye mtandao wa YouTube ni wazi SIMBA nae ana la kwake la kujivunia.

Mtandao wa VEVO wa nchini Marekani umetoa orodha ya ngoma 20 kali za wanamuziki wapya nchini Marekani ambapo collabo ya MARRY YOU ya Diamond Platnumz na Ne-Yo imeshika namba 10.

Wow!! Hakika 2017 na imeanza tena kwa ukali wake…….!!!

Mwezi uliopita Dimond Platnumz alijinadi kuwa ana mipango mikubwa mwaka huu kisha siku chache zilizopita Kiba nae akaiomba menejiment yake ya kampuni ya Sony kuachia ngoma kwaajili ya mashabiki wake ambao hawaishi kulalamika siku hadi siku.

Je, huu ndio mwanzo wa mwaka wenye ushindani zaidi kwenye Bongo Fleva hususani kwa Ali Kiba na Diamond Platnumz?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *