Staa wa Bongo Fleva na mkurugenzi mwenza wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ametoa tahadhari kwa mastaa wa muziki kwa kuwaeleza kuwa ‘soko la muziki kwa sasa limeingia kirusi’.

Staa huyo alitumia nafasi ya kumshauri staa mwenzake Shetta kwaajili ya kufikisha ujumbe kwa mastaa wengine.

Diamond amedai kuwa Bongo Fleva kwa sasa umechanganyika na siasa na hakuna tena haja ya kuimba mambo yenye maana sana ili kupata mapokeo mazuri kwa mashabiki.

Shetta ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu aachie ngoma NAMJUA ni rafiki wa karibu wa staa huyo wa WCB.

Diamond Platnumz amedai kuwa Bongo Fleva imekuwa #MzikiSiasa

‘Shetta ndugu yangu, Najua unanionea gere mwenzako toka juzi insta imehamia Madale….na wewe unataka kuingia kwenye huu upepo wa #Mzikisiasa …we usijiulize ingia tu…maana mjini sasa hivi vingoma vya Mapenzi Vigumu…ikiwezekana jifanye hata unataka kumtolea Mahali Mange Umuoe…Kesho mji wote wako…..ila kuna mawili: Sentro au Matusi – #SimbaMason,” aliandika Diamond Instagram. 

Maneno ya Diamond yamekuja siku chahche baada ya ngoma yake mpya, ACHA NIKAE KIMYA kushambuliwa kwa kuingilia mambo ya kisiasa huku akionekana kutetea upande mmoja.

Baada ya kutekwa kwa Roma Mkatoliki na utata wa ngoma ya Nay wa Mitego ‘WAPO’, ni kweli Bongo Fleva imekuwa muzikiSiasa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *