Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amekiri kuzaa na mwanamitindo wa Bongo, Hamisa Mobeto baada ya kukanusha taarifa za kuhusika na ujauzito wa mwanamke huyo kwa muda mrefu.

Diamond amethibitisha hayo leo wakati wa mahojiano na kipindi kimoja cha Radio maarufu nchini na kukiri ni kweli mtoto wa mwanamitindo huyo ni wake ila alitaka iwe siri lakini Mobeto ameshindwa kuitunza siri hiyo.

Taarifa za mwanamuziki huyo kumpa ujauzito mwanamitindo huyo zilienea katika sehemu mbali mbali nchini kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vingine.

Diamond Platnumz amesema kuwa jina alilotoa apewe mtoto wake kwa Hamisa Mobetto ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo aliamua kumwita Abdul Nassib.

Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri ili mpenzi wake Zari asijue.

Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo kwenye sherehe hiyo.

Pia Amesema pamoja na yaliyotokea alimwambia mama yake mzazi kuhusu kilichotokea amemuomba msamaha Zari na hawana shida yoyote.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *