Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa hana bifu na mwanamuziki mwenzake Alikiba isipokuwa watu wanatengeneza bifu hiyo lakini wenyewe hawana tofauti yoyote.

Diamond ameongea hayo kupitia mahujiano na kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV na kubainisha hayo leo asubuhi.

kibaking

Diamond amesema kuwa  “ Kiukweli kabisa mimi sina tatizo na Ali. Sijawahi kugombana naye na ni mtu tunaheshimiana. Kipindi Ali ndio yuko kwenye harakati za kurudi kwenye muziki ni watu walitengeza vitu kati yangu na Ali ili kutengeneza ‘attention”.

Pia Diamond ameendelea kusema “Mimi nilijua kabisa vitu ( ugomvi kati ya @diamondplatnumz na @officialalikiba ) umetengenezwa kwa hiyo nilivumilia. Labda mwenzangu alishindwa kuvumilia lakini sisi hatujawahi kugombana “ .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *