Staa wa Bongo fleva, Nasib Abdul “Diamond Platnumz”  jana amefanya show ya kufa mtu katika mji wa Mombasa nchini Kenya na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki ambao walionesha kumkubali mkali huyo kutoka ardhi ya Bongo.

Staa huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri Afrika pamoja na kimataifa ameendelea kudhihirisha ubora wake baada ya show yake kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Diamond aliandika “It’s 4:35 am now in East africa… am now going to sleep then right after waking up, will start posting my all Mombasa show Pictures…. thanks,”.

Dioamond Platnums: Akifanya show ya kufa mtu katika mji wa Mombasa nchini Kenya.
Diamond Platnumz: Akitumbuiza mashabiki katika mji wa Mombasa nchini Kenya.

Diamond Platnum kwasasa ni mwanamuziki anayefanya vizuri kutoka ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kufanya nyimbo kibao za kimataifa kulioko mwanamuziki yeyote katika ukanda huu.

Mkali huyo pia amefanikiwa kufanya kolabo tofauti na wasanii kutoka nchini Nigeria, Afrika Kusini pamoja Jamhuri ya Congo ambapo alimshikirisha mwanamuziki marehemu Papa Wemba.

chibu1

Diamond wiki iliyopita alikuwa nchini Marekani kwa ajili ya kushoot video ya wimbo wake mpya aliomshirikisha mwanamuziki nyota wa Marekani, Neyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *