Mastaa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz, Alikiba, Navy Kenzo na Vanessa Mdee wametajwa ni miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo za Africa Youth Choice Awards (AYCA).

Diamond Platnum amechaguliwa kuwania tuzo hizo katika vipengele viwili ambavyo ni msanii bora wa mwaka na msanii bora wa kiume huku Alikiba akiwa katika kipengele cha msanii bora wa mwaka.

Wakati Vanessa Mdee akiwania tuzo hizo katika kipengele cha msanii bora wa kike na kundi la Navy Kenzo lenye wasanii wawili Aika na Nareal lipo kwenye kipengele cha kundi bora la muziki.

Tuzo hizo pia zinajumuisha watu maarufu ambao wanamchango katika jamii ambapo Mama Salma Kikwete yupo katika tuzo hizo kutokana na Kampeni yake ya Mtoto wa Mwenzi ni Wako pamoja na Joyce Kiria.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa siku ya Jumamosi Septemba 17 mwaka huu  jijini Lagos nchini Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *