Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima leo amemsamehe Diamond Platnumz baada ya mwanamuziki huyo kuomba msamaha kupitia akaunti yake ya Instagram.

Gwajima leo alikuwa ameahidi kuweka wazi mambo ya Diamond Platnumz kujiunga kwake na Freemason , Lakini amedai kuwa Jana Diamond kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram Alimuomba Msamaha Kwa Mchungaji huyo.

Watu wengi leo walifurika katika kanisa hilo na wengine kutazama live kupitia Youtube wakitarajia kuwa anafunguka makubwa kuhusu Diamond.

Lakini Karibia na Mwisho wa Mahubiri yake alidai Bibilia inasema mtu akiomba Msamaha Hupashwa Kusamehewa hivyo Hata ameamua Kumsamehe na kumsitiri , lakini ametoa onyo kuwa akiendelea kumchokoza wiki ijayo atafunguka.

Gwajima na Diamond wameingia katika vita baada ya Diamond Kumuimba askofu huyo katika wimbo wake uitwao Niache nikae Kimya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *