Staa wa Bongo fleva, Nasib Abdul “Diamond Platnum” amethibitisha kwamba anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye atakuwa wa kiume baada ya mpenzi wake Zarina Hassan “Zari” kushika ujauzito.

Diamond amesema kwamba anatarajia Zari ampatie mtoto wa pili ambaye atakuwa wa kiume na anategemea kujifungua mwezi Disemba mwaka huu huku akiongeza kwa kusema baada ya kupata mtoto huyo hatoongeza tena mwingine.

tiffa

Licha ya kuenea kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba Zari hana maelewano mazuri na familia ya staa huyo lakini Diamond hakusita kusema hayo kama anatarajia kupata mtoto wa pili na mwanadada huyo raia kutoka nchini Uganda.

Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja hadi sasa ambaye anaitwa Tiffah Nassib ambapo ana umri wa mwaka mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *