Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Zuchu ambaye ni msanii wake pia chini ya lebo yake.

Diamond amesema wawili hao wamebaki kuwa kama kaka na dada na si mahusiano ya kimapenzi kama ilivyokuwa hapo awali.

Hii imekuja mara baada ya post kadhaa za Zuchu kwenye akaunti yake ya Snapchat alizoandika kuwa yupo single kwasasa na asihusishwe na kitu chochote kinachomuhusu mpenzi wake.

Kwa upande wa Zuchu naye meweka wazi kuwa kwa sasa yupo Single kupitia ukurasa wake wa Snapchat na kuthibitisha.

Mbali na hivyo Zuchu amedai kuwa hataki kuhusishwa na chochote na Mpenzi wake kwani wameshaachana na Yupo na Single.

Staa huyo ambae amekuwa akitajwa kutoka kimapenzi na CEO wa Lebo ya WCB, Diamond Platnumz huku wawili hao wakilithibitisha hilo kwa vitendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *